LOCATION:
KIMRA BARUTI
CONTACT:
supersskillsfootballclub@gmail.com
MOBILE:
0785 361 334
0654 291 932 more »



MENEJA mpya wa Manchester United Louis van Gaal anadhani atahitaji muda zaidi ili kuibadilisha timu hiyo pamoja na kukamilisha mechi sitaza kujipia nguvu kabla ya kuanza kwa msimu kwa ushindi. United ilimaliza ratiba yao ya mechi zao kujipima nguvu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Valencia jana usiku na kumpa Mholanzi huyo ambaye alichukua mikoba baada ya kuingoza nchi yake kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia, ushindi wa kwanza katika Uwanja wa Old Trafford. Sasa United wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Swansea City katika ufunguzi wa Ligi Kuu nyumbani Jumamosi lakini Van Gaal hana uhakika kama Jonny Evans, Luke Shaw na Antonio Valencia ambao hawakucheza mechi ya jana kutokana na majeruhi kama watakuwa fiti. Watatu hao wakiwa benchi, Van Gaal alilazimika kuwatumia Phil Jones, Chris Smalling na Tyler Blackett katika nafasi ya ulinzi wa kati huku Asley Young na Reece James wakicheza kama katika wingi. Akiwa amefanikiwa kufanya usajili wa wachezaji wawili pekee ambao ni Shaw na Ander Herrera kiangazi hiki, Van Gaal amesema bado anahitaji muda kwani timu wala wachezaji hawawezi kubadilika katika kipindi cha wiki mbili au tatu.
MENEJA wa klabu ya Everton, Roberto Martinez amesema dili la kumsajili winga wa kimataifa wa Ghana Christian Atsu kutoka Chelsea limekamilika. Atsu ambaye alikuwemo katika michuano ya Kombe la Dunia, msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Vitesse Arnhem ya Uholanzi na sasa amekubali kwenda tena kwa mkopo Everton. Akizungumza katika shughuli ya uzinduzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu nchini Uingereza leo, Martinez amesema anamtegemea Atsu kujiunga nao kesho kwasababu kila kitu kimeshakamilika na Chelsea. Atsu mwenye umri wa miaka 22 ataungana na Romelo Lukaku ambaye naye alitokea Chelsea na kutua Goodison Park huku mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji akiigharimu Everton paundi milioni 28.


